Kufukuzwa Kazi Sio Mwisho wa Maisha! Yaweza Kuwa Mwanzo wa Mafanikio

Image result for DONT GIVE UP

John Diebold aliwahi kufukuzwa kwenye kampuni ambayo alikuwa ameajiriwa hapo kabla kwa kutofautiana na bosi wake Mwaka 1954.
.
Hata hivyo aliamua kuanzisha kampuni yake ya The Diebold Group ambayo alikomaa nayo na cha kushangaza baada ya Miaka 3 alikuwa amefanikiwa sana na alienda kuinunua kampuni ambayo ilikuwa imemfukuza.
.
Wakati mambo magumu yanatutokea ili yatukutanishe na KITU HALISI tunachotakiwa kufanya.Kuna wakati mambo tusiyoyatarajia yanatutokea ili yatusaidie KUDHIHIRISHA UKUU ULIO NDANI yetu.
.
Usiwachukie wanaokunyima fursa,usiwachukie wanaokupinga,usiwachukie wanaokusema vibaya kuhusu Ndoto yako.Pambana kwa bidii ili siku moja waje wanunue bidhaa zako,watumie huduma ama uwaajiri.Hamishia hasira zako katika KUFANYA.
.
Kuna watu wana kufanyia mambo Mabaya leo wanadhani WANAKUKOMOA kumbe wanakutengenezea MAZINGIRA ya kufanya KITU SAHIHI KWENYE MAISHA YAKO.
.
Je,Uko Tayari kuwa kama John Diebold.
.
By: Joel nanauka

#Pambana Kuijenga Kesho Yako #Timizamalengoyako written
by: John Jonas Kiwovele - 0766-848616

1 comment:

  1. Asante San Sasa ndugu kwa mfano tusio kuwa na chakuanzia ht Mia ILi tupate njia

    ReplyDelete

Powered by Blogger.