Aina kuu 3 za marafiki ambao kila mtu anakuwa nao

Image result for AINA KUU 3 ZA MARAFIKI

Kwa Mujibu wa mwanafalsafa maarufu Aristotle,kuna aina kuu 3 za marafiki ambao kila mtu anakuwa nao:
.
1.Utility Friendship:Hawa ni wale ambao urafiki wenu umejengwa katika mahusiano yenu ya kusaidiana katika mambo fulafulani.Inawezekana mnasaidiana masomo,kazi,Fedha n.k Sifa kubwa hapa ni kuwa urafiki unadumu kwa sababu kila mmoja kuna wakati huwa anamsaidia mwenzake.
〰️〰️〰️
2)Pleasure Friendship:Urafiki huu umejengwa katika kuwa na mambo ya kiburudani ambayo mnayafurahia kwa pamoja.Mara nyingi hata kama hakuna Kitu cha maana mnachokifanya pamoja lakini starehe,hobby au interest huwa zinawaunganisha pamoja.Inawezekana mnapenda kuangalia Mpira wote,mnakutana bar kufurahia kinywaji n.k

Watu wengi hufelishwa na marafiki wa namna hii kwa sababu huwa wanawapa nafasi kubwa sana kwenye Maisha yao wakati mwingine zaidi ya wenzi wao.
〰️〰️〰️
3)Friendship for Good:Hawa ni marafiki ambao mnaunganishwa na Malengo yanayofanana na mnathamini vitu vinavyofanana(Goals and Values).Urafiki huu huchukua Muda mrefu sana kuujenga lakini ukipata mtu sahihi anaweza kuwa Msaada mkubwa sana kwenye kukusaidia kutimiza ndoto zako.Hawa hata kama hampati nafasi ya kuburudika pamoja ila Mnakuwa na malengo mengi pamoja.Wengine hata msipowasiliana kwa muda mrefu mkikutana hakuna anayemlaumu mwenzake mnakuwa kama mlikuwa wote siku zote.
〰️〰️〰️
Je,una rafiki yoyote kati ya hawa kwenye Maisha Yako.Unaweza kumtag?

by @joel_nanauka @mapambano_
See You At The Top
.
#TIMIZAMALENGOYAKO

1 comment:

  1. Asante Kwa ushauri,kumbe tunapotea Kwa kuchagua fake frinds

    ReplyDelete

Powered by Blogger.