Take One Idea and Make it Big


                   *WAZO* 
Kila wazo unaweza kulibadilisha likawa wazo kubwa na likakufanya ufanikiwe bila kujali watu wangapi tayari wanalifanya:
.
*mak juice* ni msomi aliyeamua kuuza juisi ila akatumia usomi wake kufanya kwa ubora na leo amefanikiwa sana. *Speshoz(Jeff)* ni msomi aliyeacha kazi World Bank na akatumia uzoefu wa kushona alioupata kutoka kwa mama yake na akaanza kama fundi cherehani na leo anawashonea watu wakubwa wakiwemo viongozi wa serikali na Wasanii wakubwa. *Noel Katongo @mckatongo* msomi wa ESAMI na leo Kitu Kimoja wapo anachofanya ni kuuza juice kwa namna ya ubora akitumia Elimu yake n.k @zejuice_international
.
Hii inamaanisha unaweza ukachukua wazo lolote bila kujali ni dogo au linadharaulika kiasi gani na utumie elimu uliyonayo kulifanya kuwa bora kuliko ilivyozoeleka. Tumia elimu yoyote uliyonayo kuongeza weledi wa unachokifanya. *Stumai Simba* yeye amekuja na @porridge_point,ameamua kuuza uji..ameamua kuweka weledi katika kitu kilekile ambacho wengine wamekuwa wanafanya kawaida.
.
Je, kuna wazo lolote la kawaida ambalo unaweza kuamua kuweka weledi kidogo na kulifanya chanzo cha kipato chako?
cc.
@Joel Nanauka *@mapambano_*

No comments

Powered by Blogger.